Advertisement

Thursday, 8 January 2015

PANYA ROAD KWISHA KAZI! KOVA ALALA NJE SAA 120


BAADA ya kuwakosesha amani wakazi wa Jiji la Dar es Salaam usiku wa Ijumaa iliyopita, lile kundi la vijana wahalifu linalojulikana kwa jina la Panya Road limefikia ukingoni baada ya kudhibitiwa kwa kasi kubwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Amani linakupa ‘full stori’.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kundi hilo liliibuka majira ya saa moja jioni ya Ijumaa iliyopita na kufanya vurugu katika maeneo ya Magomeni-Kagera, Dar ikidaiwa kuwa walikuwa wakilipa kisasi baada ya mwenzao aliyefahamika kwa jina la Ayubu Mohamed  ‘Diamond’ kuuawa na wananchi wenye hasira kali.

0 comments:

Post a Comment